Select Menu

.

.

RAMADHANI KAREEM

RAMADHANI KAREEM

ALLEN PETER KASIGA

http://www.loxiastudio.com/en/options/2/1#/LXModuleExport
Powered by Blogger.

Link list 3

Link list 2

Link list 1

Search This Blog

HOME

NEW HITS

UCHUMI

MICHEZO

» »Unlabelled » AFISA WA FIFA AKIRI ALIWAHIKUPOKEA RUSHWA
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Wizara ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa inayoelezea jinsi ambavyo Afisa wa zamani wa FIFA Chuck Blazer alivyokiri kuwa yeye pamoja na wenzake walipokea rushwa ikiwa ni pamoja kuichagua Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa fainali ya kombe la dunia mwaka 2010.
Katika taarifa hiyo imeweka wazi mtandao wa malipo ya rushwa ulivyokuwa ukifanywa ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA, taarifa zinazoegemea uchunguzi uliofanywa na shirika la kijasusi la Marekani FBI.
Taarifa hiyo ambayo inamwelezea Afisa huyo wa zamani wa Fifa Chuck Blazer kukiri kupokea rushwa sasa huenda ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa inayoindamana shirikisho la FIFA.Mmerakani huyo kwenye taarifa hiyo inadai alikuwa ni mmoja wa watu walioisuka mipango ya kupokea rushwa katika tukio jingine la fainali la kombe la dunia 1998.
Taarifa za Kukiri zipo katika maandishi wakati wa kesi yake mwaka 2013 wakati ilipokuwa akisikilizwa katika mahakama ya Easten New York huko Marekani ambapo alikiri makosa kumi yaliyokuwa yanamkabili.Blazer alikuwa afisa wa ngazi juu wa FIFA eneo la kanda ya Amerika Kaskazini na Kati na ukanda wa nchi Caribbean kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2011.
Marekani imefungua kesi ya rushwa inayowakabili maafisa wa FIFA jambo lililofanya Rais wa FIFA Sepp Blatter kuamua kutangaza kujiuzulu.Mwendesha mashtaka wa Marekani wiki iliyopita aliwashtaki maafisa 14 wa ngazi wa juu wa FIFA tuhuma za rushwa.

About G'14

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply