Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw paul Makonda anaamini kipaji ni ajila na ndio maana ameamua kuandaa shindano la kusaka vipaji linalokwenda kwa jina la Kinondoni Talent Search litakalofanya katika wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam.
Lengo kuu la shindano hilo kutoa fulsa kwa vijana wa kinondoni kutumia vipaji walivyonavyo kupata kipato kitakachowaendeshea maisha yao.
Fulltainment imeongea na moja kati ya judge wa shindano hilo MC Pilipili amesema kwamba katika shindano hili hawana vigezo vyovyote vitakavyomfanya mtu ashiriki ila kigezo kikubwa ni kwamba unatakiwa uwe ni mkazi wa wilaya ya kinondoni.
pia ameongeza kwa kusema kwasasa wanaenda kuingia katika hatua ya pili ya kuanza kuwachuja washiriki waliochukua form za kujiandikisha baada ya kukamilika kwa zoezi la uchukuaji form kwa washiriki.
Zoezi litaanza rasmi jumatatu 11.05.2015 saa 2 asubuhi pale coco beach jijini Dar es salaam wote mnakaribishwa kuja kushuhudia vipaji vilivyopo kinondoni
No comments