Baraza la Sanaa Tanzania BASATA wamesema kwasasa ni ruksa kwa mtu yoyote au shirika lolote ambalo linawazo la kuanzisha Tuzo nyingine za muziki hapa Tanzania wajitokeze ili waweze kushirikiana nao katika kukuza muziki wa Tanzania.
Afisa habari wa Basata Bw KWIZELA amesema kuwa hakuna sababu ya kuwepo kwa tuzo moja ya Kilimanjaro peke yake hapa Tanzania ikiwa uwezekano wa wadau wengine kuanzisha tuzo nyingine za muziki upo,kwahiyo kwa mtu yoyote mwenye wazo la namna hiyo ajitokeze na aende Basata wao wako tayari kushirikiana nae na kumsaidia mawazo zaid ili kufanikisha kuendeleza mziki wa Tanzania.
BASATA WARUHUSU KUANZISHWA TUZO NYINGINE TZ
Inafahamika Basata ndio wamiliki wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards na ndio wanaosimamia shuguli zote za uendeshaji wa Tuzo hizo kila mwaka.
Mratibu wa tuzo kutoka basata amesema kuwa wasanii wanatakiwa wajisajili ili waweze kutambulika kwasababu mwakani watakaoruhusiwa kushiriki kwenye tuzo zozote ni wale wasanii waliosajiliwa tu
No comments