Mwanamuziki wa RnB
Christina Milan amethibitisha zile story za chini kwa chini wa siku nyingi kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na
msanii wa muziki wa Rap LilWayne ambaye pia anamwakilisha katika kampuni yake
ya Young Money Entertainment.
Wawili hao walionekana pamoja katika
pigano la karne kati ya Bingwa Floyd Mayweather na Manny Paquiao mjini Las
Vegas.
Katika mahojiano na mtandao wa
Etonline, Milian alisema kuwa Wayne ni mtu muhimu sana kwake
''Ni mtu muhimu sana kwangu,ninaishi
naye huru na sote tunafurahia'',.alisema.''Hakuna kitu kizuri kama kuwa na
hisia na mtu hatua ambayo inakufanya kutojali kitu ambacho watu wengine
wanasema,ni hisia ambazo watu uhisi kwa kweli'',.
Na alipoulizwa kuhusu kuolewa na Lil
Wayne alisema:''huwezi kujua,ninamaanisha kwamba penzi huchochea vitu vizuri
kama hivyo'', alisema Milian aliyejawa na tabasamu.
No comments