Mama mzazi wa Banza Stone ameieleza full news tz kuwa hali
ya mwanae inazidi kuwa mbaya siku hadi siku na sasa Banza amegoma kula kabisa kwa siku ya 3 sasa.
Akiongea na kipindi cha Ubaoni cha Gardner juzi kupitia E FM mama wa Banza alisema banza amegoma kula
kabisa kwa siku tatu mfululizo hali chochote wala hanywi chochote,
Kwa mujibu wa kaka yake na Banza Jabir Masanja alisema Banza anasumbuliwa
na fangasi kichwani kwake na dawa anazotumia ni kali sana kiasi cha kumpotezea
hamu ya kula
Mama huyo ameongea kwa masikitiko na kusema mpaka sasa
hakuna msanii mwezake yoyote ambae ameenda kumuangalia wala kumjulia hali na yeye kama mama hawezi kuwalaumu kwanini wasanii wenzie hawaendi kumuangalia
kwasabu kila mtu ana moyo wake,amesema kwasasa yeye kama mzazi ataendelea na
kumuuguza mwanae mpaka mwisho.
Jabiri amewaomba wadau wa muziki na mashabiki wa Banza
walioguswa kumchangia chochote Banza kwa kutuma chochote kutumia namba
0715407088 au 0753786016
No comments