Ali Nipishe akiongea na fullnewstz amesema sababu za ukimya wake wa mda mrefu ulisababishwa na matatizo aliyoyapataa baada ya kununua Gari ya wizi ambayo ilimsababishia kufungwa jera kwa miezi 3 kutumikia adhabu yake baada ya kesi yake kufika katika mikono ya sheria.Gari hiyo ilikuwa na aina ya ALTEZZA ambayo alienda kuinunua Zanzibar baada ya kufanyiwa mipango na mpenzi wake aliekuwa nae kimapenzi ambae alikuwa anaishi Zanzibar.
Kwasasa Ali Nipishe ameshatoka na kesi yake imeisha na amerudi tena kwenye mziki kama kawaida.Ali nipishe alieleza zaidi wakati akiongea na Full News Tz kwamba kwa sasa anasimamiwa na Papaa Misifa akiwa katika uongozi mpya ingawa THT ni nyumbani ataendelea kuwa nao pamoja kama kawaida.
Video ya ngoma hiyo imeshakamilika na muda sio mrefu kutoka sasa itaachiwa kupitia vituo vya television.
No comments