Kwa mujibu wa Tume iliyopewa kazi ya kuchunguza ajali hiyo ilitoa taarifa kuwa Mv Bukoba kabla ya ajali meli hiyo ilikuwa na abiria kati ya 750 - 800 pamoja na wafanyakazi 37.Kati ya hao waliookolewa wakiwa hai ni 114.
Huku miili 391 ilipatikana na kuzikwa katika makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza na baadhi ya marehemu walichukuliwa kwenda kuzikwa na ndugu zao .Hata hivyo jumla ya miili ya watu 332 haijapatikana mpaka leo.
Leo katika kanisa la Mtakatifu Francis Nyakahoja jijini Mwanza. Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata ni mmoja kati ya watu waliopoteza wazazi na ndugu kupitia ajali hiyo, hivyo kupitia Foundation yake amewajumuisha marafiki zake kushiriki ibada hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya matukio kadhaa ya kijamii likiwemo suala la kuzikumbusha Mamlaka husika kuzingatia sheria za usafiri majini.
Katika ibada hiyo Flaviana atajumuika na wanamuziki wa Bongo Fleva kama Mwana FA, Fid Q, Ay, Damian Soul, One Inclidible na mshindi wa Big Brother Africa Idrisa Sultan
No comments