KUFUATIA malumbano ya ‘team’ kwa wasanii wenye ugomvi,MTUMBUIZAJI BORA WA MUZIKI WA MWAKA WA KIKE ambae pia ni MWIMBAJI BORA WA KIKE BONGO FLEVA
Vanessa Mdee ‘V Money’ ameibuka na kukemea makundi hayo akidai hayana faida yoyote kwa jamii na kwa sanaa za wasanii husika.Alisema makundi hayo yanaharibu sifa ya msanii, kazi zake na yanaongeza chuki badala ya kuleta furaha na mafanikio ya msanii.
NUKUU “Kama mashabiki wanapenda kazi zangu waendelee kunipenda na waonyeshe ushirikiano nami kwa wasanii wengine, lakini masuala ya timu, timu sitaki, hazina maana kwa jamii,” alisema Vanessa.
Vanessa, anayemiliki tuzo mbili za Kili, ikiwemo tuzo ya mtumbuizaji bora wa mwaka wa kike na mwimbaji bora wa kike Bongo Fleva, aliongeza kwa kuwataka wasanii walioanzisha ‘team’ waachane nazo, ili wajiongezee mashabiki badala ya kuwagawa
No comments