Reality Tv star Kylie Jenner (17) amesema kuwa mama yake mzazi aliacha kumpatia pesa za matumizi akiwa na umri wa miaka 14
Kuanzia hapo alikuwa anajitegemea mwenyewe kwa kila kitu kuanzia mafuta ya gari yake na chakula chake kwa ujumla.
Kylie ambae kwa sasa anamiliki vitu vingi vya dhamani ikiwemo nyumba ya dhamani ya dola milioni 2.5 na gari ya dola 125,000 amesema vitu vyote hivyo amevipata kwa juhudi zake mwenyewe
Kylie ambae anaingiza pesa nyingi kupitia kipindi chake cha KEEPING UP WITH THE KARDASHIANS na pia anabidhaa nyingi chini ya jina lake zikiwemo rangi za kucha na make up anasema kwamba anapenda vitu vizuri lakini anaweza kuishi bila vitu hivyo
No comments