Kuna tofauti kubwa kati ya chama cha ACT TANZANIA na ACT WAZARENDO
hilo lazima lieleweke kwa waTanzania wote.
Leo mwenyekiti mkuu wa ACT Tanzania Bw KADAWI LUCAS LYMO ameweka wazi kila kitu
kinachoendelea kati ya vyama hivi viwili vya siasa. KADAWI LUCAS LYMO ambae ni mwenyekiti wa ACT TANZANIA amesema kwamba chama chake kilisajiliwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za usajili wa chama na msajili mkuu wa vyama vya siasa na alipewa barua ya usajili 4/11/2014 ingawa chama chake kilianzishwa rasmi tarehe 11/11/2013
Kutokana na hilo ameamuwa kuweka wazi sekeseke linaloendelea sasa baada ya kuanzishwa kwa chama kingine cha ACT WAZALENDO ambacho kinaongozwa na Zitto kabwe na team yake,kwa mujibu wa maelezo ya Lymo amesema kuwa chama cha wazalendo ni chama batili ambacho kimepewa usajili kimakosa ambapo anashangazwa na msajili mkuu wa chama amekiuka sheria za usajili wa chama kwa kukisajili chama hicho ambacho kinalengo la kuwapoteza wananchi
NUKUU
Chama cha wazalendo ni chama cha
watu ambao ni waroho wa madaraka ambao wanalengo la kupata madaraka ambayo si
ya kuleta maendeleo kwa nchi bali ni kujinufaisha wao wenyewe na familia zao.Bwana Kadawi pia amewataja wachawi wake ambao ni wanaokipotezea malengo na muelekeo chama chake katika na kusema kwamba wachawi hapo ni msajili mkuu wa vyama vya siasa na bwana Zitto kabwe na amewaomba waTanzania kuwa watulivu wasibiri mahakama ifanye kazi yake maana tayari swala liko mahakamani.
Na mwisho kabisa bwana kadawi ambae ndo mwenyekiti wa ACT TANZANIA amesisitiza kuwa chama chake bado usajili wake uko hai na kinaendelea kufanya kazi.
No comments