Dokta amempiga stop staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel kwenda kujifungulia nchini Marekani kwa sababu hali yake ya ujauzito aliyofikia haruhusiwi kusafiri kwa kutumia usafiri wa anga kwenda popote.
Chanzo makini cha GPL kilisema kuwa, Aunt alijiwekea mpango wa kwenda kujifungulia nchini huko kwa muda mrefu lakini alikuwa akisubiri mimba ikue kidogo kitendo ambacho hakikutakiwa kwa kuwa ujauzito umekuwa mkubwa na kusafiri kungemletea tatizo la presha ya kushuka.
“Imebidi nikubaliane na daktari alivyosema kwa kuwa wao wanajua hivyo siwezi kupingana nao naogopa nisije kupata matatizo, bora nijifungulie hapahapa nyumbani na nimelikubali hilo na mawazo ya nyuma nimefuta japokuwa nilikuwa nimeandaa kila kitu kwa safari hiyo,” alisema Aunt alipopigiwa simu na FULLTAINMENT
Awali Aunt alipanga kwenda kujifungulia nchini Afrika Kusini lakini baadaye aliahirisha baada ya kupata shavu kwa marafiki zake waishio nchini Marekani waliomtaka kwenda kujifungulia huko na kukaa kwa miezi mitatu.
DOCTOR AMZUIA AUNTY KWENDA KUJIFUNGUA MAREKANI

No comments