Timu ya taifa ya wanawake ya England
imeanza vibaya mashindano ya kombe dunia kwa upande wa wanawake yanayoendelea
nchini Canada, kwa kukubali kipigo cha bao moja kwa yai viza kutoka kwa
Ufaransa kwenye mtanange uliopigwa hapo jana.
Takriban
dakika 29 tu za mchezo huo zilitosha kwa mwanadada Eugenie Le Sommer kupeleka
msiba kwa timu ya England umbali wa yadi 20 tu.
Matokeo
haya yanaendeleza ubabe wa taifa la Ufaransa kwa upande wa soka la wanawake,
ambapo takribani miaka 41, England haijafanikiwa kuwashinda wapinzani wao hao.
Na
katika viwanja vingine Hispania ilicheza dhidi ya Costa Rica,matokeo ni moja
moja…. Nayo Colombia ilivaana na Mexico, katika kipute hicho Colombia na Mexico
nayo, moja moja. Na hatimaye Brazil walifumania nyavu mara mbili na korea ya
kusini waliondoka kichwa chini
No comments