Wanafunzi wa chuo kikuu cha Mlimani UDSM wamegoma kuingia madarasani na kuendelea na masomo yao huku
wakihishinikiza serikali kuwalipa fedha zao za kujikimu kimaisha.
Akizungumza baada ya mgomo huo Raisi wa chuo hicho KIJAPONDA AHADI amesema kutokana
mkataba baina yao na serikali fedha hizo
zinatakiwa zilipwe baada ya wiki 8
lakini mpaka sasa wameingia wiki ya 11
bila kuwepo kwa malipo hayo.
Aidha amesema tatizo hilo limekuwa likijirudia mara
kwa mara na kuwasababishia usumbufu mkubwa ili hali serikali ikiwa inatambua
mtu awezi kuishi bila kuwa na fedha ya kujikimu.
Kwa upande wake Waziri wa mikopo wa chuo hicho SHIFUNDI BERNAD amesema kimsingi
matatizo hayo yanatokana na mfumo mbaya wa mamlaka yenye dhamana ya kukusanya
fedha za mikopo kwa walioajiriwa .
No comments