Mo music
ambae ametoa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la NITAZOEA ameiambia
Fulltainment kwamba ametokea kumpenda sana mrembo wa bongo movie LULU MICHAEL
kutokana na umahiri wake katika kazi zake za filamu,ameongeza kwa kusema maana uwezo wake una
tofauti kubwa na waigizaji wengine wa kike.
Mo music
ameongeza kwamba huwa ana kawaida ya kutazama filamu za wasanii mbali
mbali lakini za lulu humvutia zaidi kiasi
kwamba anatamani amshirikishe kama video queen katika moja ya kazi zake za
mziki.
NUKUU:
Ninafuatilia kazi mbali mbali ,ila kwa Lulu ni tofauti natamani nimshirikishe
katika video ya wimbo wangu mpya Nitazoea kwakuwa naamin ana mvuto mkubwa.
Alimaliza mo music.
No comments