Aidha serikali
kupitia kwa waziri wake wa maswala ya kigeni ameiambia BBC kuwa mazingira
yataruhusu uchaguzi huru na wa haki.Waziri wa mambo ya nje wa Burundi
ameihakikishia jamii ya kimataifa kuwa taifa lake litaandaa uchaguzi huru na wa
haki.
Akiongea wakati wa
mkutano wa muungano wa Afrika nchini Afrika Kusini bwana Alain Aime Nyamitwe
amesema kuwa hali ya kisiasa nchini humo imeimarika na vyama vyote kwa sasa
vinaendelea na kampeini tayari ya kuchaguzi.Kuhusiana na suala la waangalizi wa
uchaguzi wa kimataifa kususia uchaguzi huo, waziri huyo amekariri kuwa zoezi
hilo linahusisha raia wa burundi na wala sio waangalizi.Hata hivyo amesema kama
taifa lolote huru, wao wametoa mwaliko kwa makundi yote na uamuzi ni wao ikiwa
watakwenda Burundi au la.
Wakati huo huo
amesema serikali ya rais Pierre Nkurunziza wako tayari kuendeleza mazungumzo ya
viongozi wa upinzani ili kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki, ila tu ni
wapinzani ndio wanaohujumu mpango huo.Wakati huo huo rais wa Zimbabwe Robert
Mugabe ameonya wakuu wa serikali dhidi ya kuanzisha machafuko kwa kuwania zaidi
ya mihula miwili.
Onyo hilo
lilionekana kuelekezwa kwa rais wa Burundi ambaye anawania muhula wa tatu licha
ya pingamizi kutoka kwa upinzani kuwa ametumikia mihula miwili.Rais Nkurunziza
amekariri kuwa muhula wa kwannza ulikuwa kipindi cha mpwito.
Rais mugabe
anahudumu muhula wa saba lakini wa kwanza chini ya katiba mpa ya Zimbabwe,
inayowashurutisha marais kuwania muhula miwili tu.Wakati huo huo Rais wa
Zimbabwe Robert Mugabe ameshutumu mataifa ya magahribi kwa kushinikiza viongozi
wa bara la Afrika kuhudumu mihula miwili pekee
No comments