Wale atoa Album mpya The Album About Nothing.
Olubowale Victor Akintimehin a.k.a Wale ameachia albam yake mpya inayokwenda kwa jina la The Album about Nothing Hii ni albam yake ya 4 ambayo imeanza kutayarishwa 2013 na kukamilika 2015. Moja kati ya mikono iliyohusika kutengeneza album hii ni kama Dj Khalil, Rex Kudo, Idan Kalai ,Sonny Digital ,Jake One,No Credit na Pro Reese.
Albam hii meingia sokoni March 31 ,2015 nakupokelewa vizuri na mashabiki wa music . Imefanikiwa kushika namba moja kwenye chati za billboards baada ya kuuza nakala laki 1 wiki ya kwanza .Nyimbo The Body aliyo mshirikisha Jeremih ilitoka kama utangulizi wa album na imefanya vizuri sana katika chart mbalimbali za music.
Usher ,Jeremih ,J.cole na SZA ndo majina pekee yalio shirikishwa kwenye album hii.
Bonyeza link hapo chini kusikiliza wimbo wa Body aliomshirikisha Jeremih
https://www.youtube.com/watch?v=zQMMI8itli8

No comments