RAMADHANI KAREEM
ALLEN PETER KASIGA
http://www.loxiastudio.com/en/options/2/1#/LXModuleExport
Powered by Blogger.
Link list 3
- MICHEZO (1)
Link list 2
Link list 1
Search This Blog
HOME
NEW HITS
UCHUMI
MICHEZO
Toka mapema asubuhi ya leo kupitia mitandao ya kijamii tuliona tangazo linaloonyesha kuwa leo kwenye xxl ya clouds fm kutakuwa na supplies
DJ D OMMY a.k.a WASHAWASHA amesikika kwa mara ya kwanza kwenye show hiyo mida ya saa 8 mchana
Pia D Ommy alielezea furaha yake ya kupata nafasi ya kujiunga na familia ya XXL na kusema alikuwa anatamani siku nyingi sana kupata mchongo huo lakini muda ulikuwa bado haujafika,Hatimae ndoto yake imetimia rasmi leo
Mkali wa Bongo Fleva Madii kutoka tip top connection ameelezea mambo ambayo atakuwa anayafanya katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani,
Kwanza kabisa amesema hiki ni kipindi ambacho anatumia muda wake mwingi kukaa na marafiki kuongelea mambo yanayohusiana na dini yao na kuhimizana katika kufunga na kufuata matakwa ya dini ya kislamu.
Pia na yeye amekuwa ni moja ya wasanii ambao kwa mwezi huu hawatofanya show yoyote kwaajili ya kwenda sawa namwezi husika.
Miongoni mwa wasanii ambao wametangaza kutofanya show kwa kipindi hiki ni pamoja na JUMA NATURE,SHILOLE n.k
Kwanza kabisa amesema hiki ni kipindi ambacho anatumia muda wake mwingi kukaa na marafiki kuongelea mambo yanayohusiana na dini yao na kuhimizana katika kufunga na kufuata matakwa ya dini ya kislamu.
Pia na yeye amekuwa ni moja ya wasanii ambao kwa mwezi huu hawatofanya show yoyote kwaajili ya kwenda sawa namwezi husika.
Miongoni mwa wasanii ambao wametangaza kutofanya show kwa kipindi hiki ni pamoja na JUMA NATURE,SHILOLE n.k
Shilole ameweka wazi ratiba yake ya mwezi huu wa Ramadhani jinsi ambavyo itakuwa .
Kwanza amesema kwa mwezi huu wote hatofanya show yoyote wala hawezi kuonekana katika sehem yoyote ya starehe kama ilivyozoeleka muda wake mwingi atakuwa anautumia kuwepo nyumbani Zaidi.
Pia aliendelea kwa kusema mpenzi wake Nuu Mziwanda yuko kwao na yeye yuko kwake kwaajili ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
Kwanza amesema kwa mwezi huu wote hatofanya show yoyote wala hawezi kuonekana katika sehem yoyote ya starehe kama ilivyozoeleka muda wake mwingi atakuwa anautumia kuwepo nyumbani Zaidi.
Pia aliendelea kwa kusema mpenzi wake Nuu Mziwanda yuko kwao na yeye yuko kwake kwaajili ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani
Filamu ya Kuelimisha jamii Inayojulikana kama DESIRE TO SUCCEED kuzinduliwa Siku ya Jumamosi tarehe 25 Juni 2015, Saa 12.00 Jioni katika ukumbi wa CENTURY CINEMAX Dar Free Market.
MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Rose Ndauka pamoja na wasanii wengine wakali katika tasnia ya filamu wameshiriki katika sinema maalum kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu huduma za Benki ya DCB Commercial Bank ambapo wateja wa Benki hiyo na wateja wapya watatambua huduma na faida zitokanazo na taasisi hiyo ya kifedha.
Commercial Bank, ikishirikiana na Kampuni ya Consnet Group imeandaa Filamu maalumu ya Kiswahili inayoitwa DESIRE TO SUCCEED (HAMU YA MAFANIKIO) inayoelimisha na kuhamasisha wateja, wadau na umma kwa ujumla juu ya umuhimu na faida za kufanya shughuli za kibenki na DCB Commercial Bank ambazo zinabadili maisha ya mhusika.
DCB Commercial Bank imeamua kuandaa Filamu hii baada ya kutambua kuwa Watanzania wengi wanapenda kuangalia filamu za Kiswahili na hivyo inaamini kuwa itaweza kuwafikia watu wengi na kufikisha ujumbe kirahisi zaidi.
“Tunashukru kwa
Benki ya DCB Commercial Bank kutambua umhimu wa wasanii kushiriki katika
kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu huduma bora zitolewazo na Benki hii, kuna
wakati watu wanaogopa kujua huduma za kibenki kupitia filamu hii watafaidika
sana,”anasema Rose Ndauka.
Moja ya changamoto zilizopo katika sekta ya benki ni jamii kukosa elimu ya kutosha juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya DCB na faida zake. Katika Filamu hii elimu, hamasa na faida mbalimbali za huduma za DCB Commercial Bank zimeonyeshwa.
Kadhalika Filamu hii inaelezea namna gani Account ya wanafunzi (DCB Student Acount) ilimsaidia Kijana Jensen kupata Elimu yake hata baada ya kufiwa na wazazi wake. Lakini pia ni namna gani baadaye kijana Jensen kwa kupitia account nyingine ya biashara (DCB Current Account) aliweza kupata mikopo ambayo ilimwezesha kufanya biashara zake kwa ufanisi na kupata faida kubwa na hivyo kuwa na msaada kwa wengine wenye shida ya fedha. Washiriki katika Filamu hii ni pamoja na Tito Zimbwe, Rose Ndauka, Jackline Pentezel, Abdul Mhema, HidayaNjaidi, Gojak na Wasanii wengine wengi.
Filamu hii
itazinduliwa siku ya Jumamosi tarehe 25 June 2015, tunategemea mgeni rasmi kuwa
ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa katika ukumbi wa
Cinema wa Dar Free Zone kuanzia saa 12 jioni hadi saa 4 Usiku ambapo wateja wa
DCB na wadau mbalimbali watakuwepo.
Baada ya
kuzinduliwa Filamu hii itaonyeshwa katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dar
Es Salaam yakiwemo City Center, Magomeni, Arnautoglu Mnazi Mmoja, Tabata,
Temeke, Ukonga, Chanika, Mabibo and Kariakoo kuanzia tarehe 26 June 2015 hadi
tarehe 14 Agusti 2015. Katika Uzinduzi rasmi DVD za filamu hii itauzwa kwa Shs
10,000. Filamu hii inasambazwa na kampuni ya Jasons Productions ya Jijini Dar
Es Salaam. Kiingilio katika uzinduzi huo ni Bure.
Katika maeneo yote
ambayo Filamu hii itaonyeshwa Wadau mbalimbali watapata nafasi ya kufungua
akaunti mbalimbali zinazotolewa na DCB Commercial Bank kufuatana na mahitaji
yao kama vile Akaunti za Biashara, Wanafunzi, Watoto, Akiba za watu binafsi,
Vikundi, makampuni nk.
Mkali aliyeshirikishwa kwenye ngoma ya Davido
“Fans Mi” Philly rapper Meek Mill wameongezwa kwenye list ya wasanii ambao
watapamba usiku wa tuzo za BET 2015, ikiwa ni tuzo za 15 za katikati ya mwaka
2015. Meek Mill na Ne-Yo wanaongezea ukali katika list ya wakali kama
Kendrick Lamar, Chriss Brown na Meek Mill atashare stage na
Nick Minaj.
Kwa watangazaji wa siku hiyo ni pamoja
na Zendaya, Michael B.Jordan na Laverne Cox wa Netflix hit Orange is the new
black.Mastaa kutoka Marekani Tracee Ellis-Ross na Anthony Andreson ndio watakuwa hosts wa usiku huo, Juni 28
Uongozi wa Azam FC upo katika hatua za mwisho
kumsajili mlinda lango wa Jeunesse ya Ivory Coast Vincent Atchouailou de Paul
Angban.Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili wiki ijayo
akiambatana na Kipre Tchetche, Kipre Bolou, na Serge Wawa Pascal kwa ajili ya
kusaini Mkataba wa kujiunga na Azam FC.
Mlinda mlango huyo aliyezaliwa Februari 2,
mwaka 1985 mjini Anyama, pia amewahi kufanya majaribio na kucheza kwenye timu
ya wachezaji wa akiba wa Chelsea ya England.Kipa huyo aliyeibukia katika klabu ya vijana ya Rio Sport d’Anyama amwewahi chezea klabu ya Sawe Sports msimu wa 2006/2007, ASEC Mimosas
2007/2009 kabla ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Daniel Yeboah.
Amewahi kudakia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Ivory Coast katika michuano ya Afrika nchini Benin mwaka 2005 na aliiwakilisha pia nchi yake katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008
Kwasasa Wema yuko singida ambako anaendelea kuhamasisha vijana wajiandikishe katika daftari la kupiga kura na hapo hapo pia wema amesema tayari kampeni za chini chini zimeshaanza.
Tarehe 14 mwezi 07 fomu zitaanza kutoka kwa wale wanaotaka kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo,wema amesema tarehe 15 mwezi ujao atarudi singida kwaajili ya kuchukua fomu rasmi
Mama mzazi wa Banza Stone ameieleza full news tz kuwa hali
ya mwanae inazidi kuwa mbaya siku hadi siku na sasa Banza amegoma kula kabisa kwa siku ya 3 sasa.
Akiongea na kipindi cha Ubaoni cha Gardner juzi kupitia E FM mama wa Banza alisema banza amegoma kula
kabisa kwa siku tatu mfululizo hali chochote wala hanywi chochote,
Kwa mujibu wa kaka yake na Banza Jabir Masanja alisema Banza anasumbuliwa
na fangasi kichwani kwake na dawa anazotumia ni kali sana kiasi cha kumpotezea
hamu ya kula
Mama huyo ameongea kwa masikitiko na kusema mpaka sasa
hakuna msanii mwezake yoyote ambae ameenda kumuangalia wala kumjulia hali na yeye kama mama hawezi kuwalaumu kwanini wasanii wenzie hawaendi kumuangalia
kwasabu kila mtu ana moyo wake,amesema kwasasa yeye kama mzazi ataendelea na
kumuuguza mwanae mpaka mwisho.
Jabiri amewaomba wadau wa muziki na mashabiki wa Banza
walioguswa kumchangia chochote Banza kwa kutuma chochote kutumia namba
0715407088 au 0753786016
Subscribe to:
Posts (Atom)
Recent Comments